Wilaya ya Ileje imepokea jumla ya matenki 50 yenye thamani ya Tzsh.Milioni 25 toka Kampuni ya AFRiCAB ukiwa ni mchango kwaajili ya kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19.
Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ofisi za Mkuu wa Wilaya yakishudiwa na Kamati ya Usalama,Wakuu wa Idara na Maafisa Watendaji wa Kata waliokuwepo kwaajili ya kupokea maelekezo ya ugawaji wa vitambulisho vya wajasiliamali.
Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo Mkuu wa Wilaya alimshukuru mdau huyo huku akiomba wengine kuweza kujitokeza katika kusaidia jamii akiwaagiza Watendaji wa Kata,vijiji na wanachi kwa ujumla kutunza vifaa hivyo na kuhakikisha vinafanya kazi iliyokusudiwa
Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Ndg.Deo Rwakagera alisema kuwa waliamua kutoa msaada huo kwa vile wao ni wadau wa maendeleo na wanapenda kuona afya za Watanzania zikiendelea vema.
Mkurugnzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg.Haji Mnasi aliahidi kuhakikisha matenki hayo yanafika kwenye maeneo husika ili kuanza kutumika mara moja.
Kwa mujibu wa kikao hicho maeneo yanayotarajia kupata msaada huo ni kwenye maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu kama vile masoko,minada ,shule na baadhi ya nyumba za ibada.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa