Na;Daniel Mwambene,Ileje-Songwe
Wadau wa elimu wilayani Ileje mkoani Songwe wametakiwa kuirejesha wilaya hiyo katika mstari baada kuwaendelea kufanya vibaya katika mitihani ya kitaifa.
Wakizungumza katika kikao cha Wadau wa Elimu kilichofanyika katika ukumbi wa CCM mjini Itumba wadau waliomba kuweka uzalendo mbele ili kuikwamua wilaya yao iliyokuwa iking'ara kitaaluma kwa shule za msingi zaidi ya miaka 15 iliyopita.
Wamesema kuwa kinachotakiwa ni kuvaa uzalendo kwa kila mdau na kuchukua hatua zenye kuleta matunda cha ili kuiweka Wilaya ya Ileje katika nafasi nzuri kitaaluma kwa ngazi mbalimbali za elimu.
Mwenyekiti wa Chama cha Walimu wilayani humo Ndugu Robert Simbeye aliomba wasimamizi wa utekelezaji maazimio ya vikao kuhakikisha wanafutilia hatua kwa hatua utekelezaji wa maazimio hayo ili kueka kurudia kujadili mambo yaliyokwisha jadiliwa na kuwekewa mikakati.
Pia kiongozi huyo alikemea walimu wanaojihusisha kufanya mapenzi na wanafunzi kuwa ni sawa na kuku anayekula mayai
anayoatamia.
Akitolea mfano wa mwalimu wa Sekondari ya Lubanda aliyehukumiwa kwenda jela miaka 30 hivi karibuni Mwalimu Simbeye alisema kuwa vitendo kama vile havimwaibishi mwalimu mhusika tu bali aibu hiyo huelekea kwa walimu wote.
Naye mdau mwingine kutoka vyama vya siasa ndugu Anania Mtawa aliomba juhudi ziongezwe katika kuzalisha wanafunzi wa masomo ya Sayansi ili kuwawezesha vijana kupata fursa za ajira katika Tanzania hii ya viwanda.
Mzee Mtawa aliongeza kuwa,unatakiwa mpango mzuri na wa wazi juu ya ulinzi wa shule kuliko ilivyokuwa siku chache zilizopita ambapo walinzi wa shule walikuwa wakiwabana Walimu Wakuu wakidai malipo yao hali iliyokuwa ikipelekea baadhi yao kutoa fedha za mfukoni ili kuondokana na usumbufu.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe.Ubatizo Songa aliiwataka wadau hao kuelekeza macho yao katika shule ya Sekondari ya Ileje iliyokuwa ikihudumiwa na wilaya kabla ya kila kata kuwa na shule yake.
Alisema kuwa shule hiyo yenye Kidato cha Tano na Sita pia huchukua wanafunzi wa kutwa kutoka kata za Itumba na Isongole ambazo pia zina shule zao.
Hata hivyo katika kikao hicho kilichokuwa chini ya uenyekiti wa Mkuu wa Wilaya Mhe.Joseph Mkude taarifa aliyosomewa kutoka Idara ya Sekondari ilionesha shule binafsi za Consolata,Mbagatuzinde na Shangwale zimefanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa Kidato Cha Pili zikilinganishwa na shule za serikali.
Kufuatia hali hiyo Mwenyekiti wa kikao alilazimika kucheua nyongo kwa Wakuu wa Shule za Sekondari za Mbebe,Kakoma,Stivin Kibona,Mlale na Lubanda ambazo matokeo yake hayakuwa mazuri na amekuwa akiwaonya kuhusu utendaji wa kazi.
Nyongo hiyo iliyocheuliwa na kiongozi huyo haikuicha salama Shule ya Sekondari ya Ileje ambayo ina ziada ya walimu wa sanaa ambapo aliagza mamlaka zinazohusika kuwapangia vituo vingine.
Katika kuhakikisha usimamizi wa taaluma unakwenda vema Mhe Mkuu wa Wilaya ameagiza idara hiyo kuacha maafisa watatu Ofisini na kuwataka wengine kwenda vijijini kuhudumia wananchi.
Kwa miaka ya hivi karibuni Wilaya ya Ileje imekuwa ikifanya vibaya katika mitihani ya Taifa tofauti na miaka kadha iliyopita ambapo kuubeba mara kadhaa mkoa wa Mbeya kabla ya mkoa huu wa Songwe kuanzishwa.
Uchunguzi katika kata kahaa umebaini juu ya kuwepo kwa miundombinu isiyo rafiki kwa walimu na wanafunzi kutokana na kuchakaa na kupelekea Halmashauri ya Wilaya hiyo kuchukua hatua za kuijenga upya ikiwemo shule ya Yenzebwe iliyopo Kata ya Itumba.
Wakizungumza nje ya kikao hicho baadhi ya wajumbe waliunga mkono kauli ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mhe Ubatizo Songa kuwa ni vema kuongeza wigo wa wadau ikiwemo kuwafuata hata walio nje ya wilaya
Mmmoja wa wadau hao toka Kata ya lubanda(?limehifadhiwa) alisema kuwa wilaya huko nje ina wasomi na wafanyabiashara ambao wakitumiwa vema wanaweza kuikwamua kielmu na kimaendeleo kwa ujumla.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa