Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Mheshimiwa Farida Mgomi, amefanya ziara za kutembelea na kufatilia mwenendo wa uchukuaji wa fomu za Wagombea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kata mbalimbali za Wilaya ya Ileje.
Katika ziara hiyo Mheshimiwa Mgomi amewasisitiza Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kuzingatia Muundo wa 4R wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Samia Suluhu Hassan ambao unalenga kuweka Majadiliano, Ustahimilivu, Mabadiliko Pamoja na Kujenga upya. Huku lengo kuu Likiwa ni kufanyika kwa uchaguzi huru na wa Kidemokrasia kwa watanzania wote.
Aidha Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ametoa rai kwa wasimamizi wasaidizi katika Kata, kuendelea kutoa hamasa kwa watu wenye sifa kuchukua fomu ili kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.
Zoezi la kuchukua fomu za kugombea nafasi za uongozi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa lilianza Oktoba 26, 2024 na litatamatika Novemba 1, 2024.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa