Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango wilayani hapa ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Ubatizo Songa imetoa maagizo kwa Wataalam Idara ya Maendeleo ya Jamii kuongeza msukumo kwenye ukusanyaji wa madeni ya mikopo ya asilimia kumi iliyotolewa kwa Vijana, Wanawake na watu wenye ulemavu.
Ikumbukwe mikopo hiyo ilisitishwa ili kupisha utaratibu mpya ambao utatolewa na Serikali wenye lengo la kuongeza tija zaidi kwa wanufaika wa fedha hizo.
Maagizo hayo yametolewa leo Machi 20, 2024 katika Kikao cha FUM kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ambacho kinahusisha Waheshimiwa Madiwani wa Kata zote pamoja na Wakuu wa Idara.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa