Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mheshimiwa Farida Mgomi, amewaongoza Wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Wilaya, Wakuu wa Taasisi za Serikali pamoja na Wakuu wa Idara katika Halmashauri ya Wilaya ya Ileje kutoa msaada na mahitaji kwa Wafungwa katika Gereza la Wilaya ya Ileje.
Msaada huo umekabidhiwa mapema leo February 10, 2025 ambapo Dc Mgomi amesema msaada huo ni sehemu mojawapo ya kuigusa Jamii na Makundi yenye uhitaji ikiwemo Wafungwa, Msaada uliokabidhiwa siku ya leo ni pamoja na Sabuni za Kuogea Boksi Saba, Mchele Kil0 50, Mafuta ya kupikia Lita 5, Mafuta ya Kujipaka pamoja na Kiasi cha shillingi Laki Moja Na Themanini Na Nane kwa ajili ya mahitaji mbalimbali katika Gereza .
Aidha Kaimu Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Ileje Mrakibu Mwandamizi wa Magereza (SSP) Alfred Peter Chimachi amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Ileje kwa moyo wa upendo na Ukarimu aliouonesha kwa kuigusa jamii ya wafungwa katika Gereza hilo kupitia msaada uliotolewa siku ya leo.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa