Akizungumza ofisini kwake Mhe.Gidarya amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa makarani wa sensa na kujiepusha na matapeli wa takwimu wanaoweza kutumia fursa hii kuiba taarifa za wananchi.
Ameongeza kuwa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi kwa mwaka 2022 litafanywa na makarani waliopata mafunzo huku wakiwa wamevalia vitambulisho maalum wakitumia vishikwambi maalum vilivyoandaliwa kwa zoezi hilo.
Aidha Mhe.Gidarya amewataka makarani kuzingatia mafunzo waliyoapata na kujiepusha kutoa taarifa walizozipata akisisitiza kuwa watakaobainika kufanya hivyo hatua zi kisheria zitachukua mkondo wake.
Wilaya ya Ileje ilikuwa na vituo vya mafunzo viwili kwa ya mafunzo ya zoezi hilo ambavyo ni Sekondari ya Ileje kwa wanaotoka Tarafa ya Bulamabya na Itumba kwa waliotoka Tarafa ya Bundali
Zoezi la Sensa linalofanyika kila baada ya miaka 10 hapa nchini kwa mwaka huu linafanyika masaa mahache yajayo yaani kuanzia usiku wa kuamkia tarehe 23, Agosti, 2022 likiwa mara ya mwisho lilifanyika mnamo mwaka 2012 wilaya ya Ileje ilikuwa na wakazi Zaidi ya 142000.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa