Kamati Kuu ya Siasa Wilaya ikiongozwa na Mwenyekiti wake Ndg.Patrick Ghambi iliweza kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata za Isongole,Bupigu,Kafule,Sange na Lubanda ikifurahishwa na baadhi ya miradi kwa jinsi ilivyotekelezwa ukiwemo wa ujenzi wa nyumba ya walimu katika Shule ya Msingi Ipoka iliyopo kata ya Kafule.
Hata hivyo imewataka watalaam wa halmashauri ya wilaya,mashirika ya umma,pamoja na taasisi za serikali kutekeleza mipango kazi yao kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma sawa na Ilani ya Uchaguzi inavyoelekeza.
Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Farida Mgomi akisoma taarifa ya utekelezaji kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya katika Ukumbi wa Chama uliopo Itumba (maarufu kama Kimwaga) alifafanua mambo kadhaa yaliyofanywa na serikali huku akipongeza umoja na mshikamano uliopo katika wilaya kati ya Halmashauri ya Wilaya,Serikali Kuu,taasisi,mashirika ya umma pamoja na Chama cha Mapinduzi.
Aliongeza kuwa,juhudi za Mhe.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kulijenga Taifa zimeonesha matunda na matokea makubwa katika hapo wilayani,huku akiahidi akiahidi kusimamia kwa dhati miradi yote ili kufikia malengo ya serikali katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi.
Watalaam kwa upande wao hususani kwa miradi ya Tarafa ya Bundali walieleza hali ya hewa ya mvua nyingi inayonesha kwa muda mrefu kuchelewesha kukamilika kwa baadhi ya miradi ikiwemo ya ujenzi wa miundombinu ya elimu,maji,barabara,umeme pamoja na afya.
Kumekuwa na mabadiliko makubwa ya kimaendeleo katika sekta mbalimbali wilayani Ileje ambapo tunashuhudia kwa muda mfupi ujenzi wa Vituo vya Afya vya Lubanda,Itale,Ndola ujenzi wa shule mpya msingi Lusungo,Igwiliza,Ipapa pamoja na sekondari za Shinji na Sekondari ya Wasichana ya Ileje iliopo kata ya Chitete,hii ni miradi michache kati ya mingi inayoendelea katika kila kata.
Haki Miliki Haki Zote Zimehifadhiwa